Flora mbasha biography
Flora mbasha music!
Flora Mbasha
Flora Mbasha (pia anajulikana kwa majina Flora H. Mayalah; alizaliwa katika Hospitali ya Hindu Mandhal Mwanza, 1 Juni1983) ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania.
Flora mbasha biography
Baba yake aliitwa Henry Joseph Mayala ambaye kwa sasa ni Marehemu na mama yake anaitwa Calorin Moses Kulola. [1]
Historia fupi
[hariri | hariri chanzo]Flora Mbasha ni Msukuma wa wilaya ya Sengerema katika mkoa wa Mwanza.
Flora ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya watano ambao wanne ni wa kike (Dorcus, Suzan, Esther na Flora) na mmoja ni wa kiume (anaitwa Benjamin).
Pia amekulia katika maadili ya dini ya Kikristo, wakati huo baba yake akiwa Askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God.
Babu yake na bibi yake ndio waliomlea wakishirikiana na mama yake.
Flora Mbasha alianza kuimba akiwa darasa la tatu wakati huo akienda na mama zake wadogo kwaya hadi alipokuwa na miaka kumi na tatu alipoanza kushiriki kuimba kwaya kanisani na kuimbisha baad